ProZ.com translation contests »
32nd Translation Contest: "Movie night" » English to Swahili » Entry by Mayolwa Nzala


Source text in English

Translation by Mayolwa Nzala (#37360)

To say that I was compelled by Parasite from start to finish is an understatement; its filming style with tracking shots are enthralling. Having watched several Korean films during the London Korean Film Festival, I was familiar with the usual genres employed in such films but Parasite seemed to defy them all! Parasite is comedic, in a quirky way, it is also a thriller, straddles class divisions and also depicts a family tale amongst other genres and is therefore likely to appeal to all ages.

Parasite truly deserves to be watched in a cinema to appreciate its nuances and the stylish cinematography. As a summary, to avoid spoilers, Parasite tells the tale of the interaction between the Park family and the Kim’s, an unemployed family, whose contrasting worlds collide with long lasting consequences.

[...]Bong Joon-Ho manages to pique the audience’s interest with brightly lit shots coupled with the effective use of indoor space, and it is surprising to realise, after the film’s 2 hour 12 minute length, that most of the scenes occur within the Park family’s home. The mundane elements of domesticity are displayed with an intriguing perspective showcasing Bong Joon-Ho’s flair. It is a slow burner but you will revel in its beauty and ingenuity as Parasite convinces that it operates solely on one level but it is in fact multi-layered and depicts social realism with empathy and pathos.

The cast are beguiling to watch, every facial movement and action is accentuated, even the mere act of walking up or down stairs can convey hidden meaning, which the camera fragments. Levels of unease are also created by virtue of that effective use of space with unusual camera angles and dramatic weather conditions ratcheting up that sensation. There is a surreal nature to Parasite, which its score emphasises, and furthermore the film adopts elements of the absurd devised in such an ingenious way which is truly cinematic magic. Parasite’s apparent eeriness will certainly keep you riveted and would not feel alien to the Twilight Zone school of filmmaking.

The actors are very impressive and add breadth to their roles creating relatability whilst seeming effortlessly cool. When Ki-Woo and Ki-Jeong Kim were working within the Park family home as private tutors they certainly epitomised this level of nonchalant, understated authority creating an aura of mysticism with the unspoken, almost mythical, tutoring techniques employed. Quite simply, the actors Park So-Dam and Choi Woo-Sik, as Ki-Woo and Ki-Jeong, are compelling to watch in the different directions that Parasite follows and they carry these performances seamlessly thereby inviting the audience to be on their side.

[...]Parasite is a remarkable piece of extremely skilful filmmaking, it is simply a must see film, and so I am looking forward to re-watching the film on its UK general release date.
Kusema kuwa nilivutiwa sana na filamu ya Parasite kuanzia mwanzo hadi mwisho ni kushindwa kueleza uhalisia; namna ilivyotengenezwa pamoja na picha zake fuatilizi, zilivyokuwa zinasisimua. Baada ya kutazama filamu kadhaa za Kikorea katika kipindi cha Tamasha la Filamu za Kikorea lililofanyika jijini London, nilizifahamu mbinu za kawaida zilizotumika kwenye filamu kama hizo lakini filamu ya Parasite ilionekana kuzipiku zote! Parasite inafurahisha, na katika namna isiyokuwa ya kawaida ni filamu ya kusisimua, ngumu kuichambua na husawiri mfululizo wa mbinu za masimulizi miongoni mwa mbinu zingine na hivyo kuifanya iwe na uwezekano wa kuwavutia watu wa rika zote.
Kwa hakika, filamu ya Parasite anastahili kutazamwa katika sinema ili kuzibaini vyema tofauti zake na sanaa zingine za upigaji picha na utengenezaji wa filamu. Kwa muhtasari, ili kuepuka wachafuzi, filamu ya Parasite inasimulia hadithi ya mwingiliano kati ya familia ya Park na ile ya akina Kim, familia isiyokuwa na kazi maalumu, ambapo mazingira yao tofauti yanaibua athari za kudumu.
[...]Bong Joon-Ho amefaulu kuibua raghba ya hadhira kwa kutumia picha zenye mwanga mwingi pamoja na matumizi mengi ya nafasi ya ndani na ni jambo gumu kuutambua urefu wa muda wa filamu baada ya saa 2 na dakika 12, ambao matukio mengi yanatokea katika familia ya akina Park. Vipengele vya mazingira ya nyumbani vinaoneshwa kwa mtazamo wa kuvutia unaoonesha ustadi wa Bong Joon-Ho. Ni filamu isiyokuwa ya moja kwa moja lakini utafurahishwa na uzuri na ustadi wake kwani Parasite inashawishi kuwa inafanya kazi kipekee kwa kiwango kimoja lakini kwa hakika ina filamu nyingi ndani yake na inaonesha uhalisia wa kijamii wenye hisia na huruma.
Waigizaji wanashawishi kutazama, kila mwonekano wa uso na kitendo kimesisitizwa, hata kitendo tu cha kupanda au kushuka ngazi kinaweza kuwasilisha maana fiche, ambayo kamera huigawa vipandevipande. Viwango vya kuwa na wasiwasi pia vimetengenezwa kutokana na matumizi mazuri ya nafasi na upigaji picha usiokuwa wa kawaida na hali mbaya ya hewa inayolingana na hisia hizo. Kuna uasilia usiokuwa wa kawaida kwenye filamu ya Parasite, ambao alama zake zinausisitiza na zaidi ya hayo filamu inachukua vipengele vya kuchekesha vilivyobuniwa kwa njia ya ustadi ambayo kwa hakika ni uchawi wa kisinema. Maajabu yanayoonekana katika filamu ya Parasite, kwa hakika yatakufanya ufurahie na usijihisi mgeni katika shule ya utengenezaji wa filamu za Twilight Zone.
Waigizaji wanavutia sana na wanakuza mawanda ya majukumu yao wakijenga uhusiano huku wakijipambanua. Wakati Ki-Woo na Ki-Jeong Kim wakifanya kazi katika familia ya akina Park kama wahadhiri binafsi, kwa hakika walionesha kiwango hiki cha uwezo mdogo, duni na wakijenga hali ya fumbo lisilozungumzwa, aghalabu lisiloelezeka na mbinu zilizotumika katika ufundishaji. Kwa urahisi kabisa, waigizaji ambao ni Park So-Dam na Choi Woo-Sik, kama Ki-Woo na Ki-Jeong, wanavutia zaidi kutazama mawanda tofauti ambayo filamu ya Parasite inayazingatia na wanayafanya maonesho haya kuunganika na hivyo kuwafanya watazamaji kuvutiwa na wao.
[...]Parasite ni filamu ya kushangaza iliyotengenewa kwa ustadi mkubwa, kimsingi ni filamu inayopaswa kutazamwa na kila mtu na hivyo ninajiandaa kuitazama upya katika tarehe ya kuzinduliwa kwake nchini Uingereza.


Discuss this entry